Karibu Qualitas Hospital Dental Clinic.

Idara hii imejikita katika kulinda na kurejesha afya ya kinywa kwa kutoa huduma za uchunguzi, matibabu na ushauri wa kitaalamu. 

Afya ya meno ni sehemu muhimu ya afya ya mwili mzima, ndiyo maana tunahakikisha kila mgonjwa anapata huduma salama, yenye ubora na inayozingatia viwango vya kitabibu.

Huduma Zetu:

Tunatoa huduma za uchunguzi wa meno (dental check-up) ili kubaini matatizo mapema kabla hayajawa makubwa. Pia tunahudumia matibabu ya maumivu ya meno, tooth filling kwa meno yaliyoharibika, tooth extraction pale inapohitajika, pamoja na teeth cleaning na polishing kwa ajili ya kuondoa uchafu na kulinda afya ya fizi.

Wagonjwa hupata pia ushauri wa kitaalamu kuhusu namna bora ya kutunza afya ya kinywa nyumbani.